Wednesday, June 14, 2017

TAARIFA KWA UMMA JKT IMEONGEZA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MEI 2017 KWA AJILI YA KUHUDHURIA MAFUNZO YA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2017


TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linapenda kuutaarifu umma kuwa limeongeza majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwezi Mei 2017 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 13 Juni 2017 hadi tarehe 20 Juni 2017.
Mkuu wa JKT, kwa mara nyingine tena, anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Orodha kamili ya majina ya vijana hao walioongezwa, maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz . Usomapo tangazo hili mtaarifu na mwenzio.

BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA WALIOONGEZEWA NA MAKAMBI WALIYOPANGIWA
Matokeo ya michezo mikubwa ya kirafiki hii leo.
Timu ya taifa ya Brazil ikiwa ugenini dhidi ya Australia ilitoa kipigo kikubwa cha mabao 4 kwa 0 dhidi ya Australia huku mabao ya Brazil yakiwekwa kambani na Diego Souza, Thiago Silva, Taison na Diego Souza.
Argentina nao walikuwa ugenini dhidi ya Singapore walishinda mabao 6 kwa 0 huku mabao ya Argentina yakifungwa na Fredrico Fazio na Joaquin Correa waliofunga kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili yaliongezwa mengine manne Gomez,Daniel Parades,Lucas Alario na Di Maria.
Waafrika wenzetu Bafanabafana walikuwa nyumbani kuikaribisha Zambia  na Zambia waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja huku mabao ya Zambia yakiwekwa kimiani na Brian Mwila na Lubinda Munia huku la kufutia machozi la Bafanabafana likifungwa na Lebongang Manyama.
Mabingwa wa Afrika timu ya taifa ya Cameroon walifungwa mabao 4 kwa 0 na Colombia huku mabao ya Colombia yakifungwa na Rodriguez,Yery Moina akifunga mawili na Jose Izquirero huku Cameroon wakimaliza pungufu baada ya Ndip Tambe kupewa kadi nyekundu.
Mabao mawili ya Harry Kane hayakutosha kuizuia England isifungwe mabao 3 kwa 2 na Ufaransa ambao mabao yao yalifungwa na Samuel Umtiti,Djibrii Sidibe na Osmane Dembele katika mchezo ambao Ufaransa walimaliza pungufu baada ya Raphael Varane kuoneshwa kadi nyekundu,
Profesa Kitila Mkumbo Awapa Makavu Wapinzani Wanaopinga Ripoti za Rais Magufuli
Katibu Mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewakejeli watu wanaopinga ripoti mbili za mchanga zilizowasilishwa na tume mbili tofauti za wasomi kwa Rais John Magufuli.

Profesa Kitila ambaye alikuwa mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, ametumia mtandao wake wa Twitter kufikisha ujumbe wake kwa watu aliodai wanapinga kila kitu.

“Kuna ugonjwa unaitwa opposition defiant disorder (ODD). Dalili kubwa ni kupinga kwa lengo la kupinga hadi unajipanga mwenyewe. Tuuepuke!,” aliandika Profesa Mkumbo.