Timu ya taifa ya Brazil ikiwa ugenini dhidi ya Australia
ilitoa kipigo kikubwa cha mabao 4 kwa 0 dhidi ya Australia huku mabao ya
Brazil yakiwekwa kambani na Diego Souza, Thiago Silva, Taison na Diego
Souza.
Argentina nao walikuwa ugenini dhidi ya Singapore walishinda mabao 6
kwa 0 huku mabao ya Argentina yakifungwa na Fredrico Fazio na Joaquin
Correa waliofunga kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili yaliongezwa
mengine manne Gomez,Daniel Parades,Lucas Alario na Di Maria.
Waafrika wenzetu Bafanabafana walikuwa nyumbani kuikaribisha Zambia
na Zambia waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja huku
mabao ya Zambia yakiwekwa kimiani na Brian Mwila na Lubinda Munia huku
la kufutia machozi la Bafanabafana likifungwa na Lebongang Manyama.
Mabingwa wa Afrika timu ya taifa ya Cameroon walifungwa mabao 4 kwa 0
na Colombia huku mabao ya Colombia yakifungwa na Rodriguez,Yery Moina
akifunga mawili na Jose Izquirero huku Cameroon wakimaliza pungufu baada
ya Ndip Tambe kupewa kadi nyekundu.
Mabao mawili ya Harry Kane hayakutosha kuizuia England isifungwe
mabao 3 kwa 2 na Ufaransa ambao mabao yao yalifungwa na Samuel
Umtiti,Djibrii Sidibe na Osmane Dembele katika mchezo ambao Ufaransa
walimaliza pungufu baada ya Raphael Varane kuoneshwa kadi nyekundu,
0 comments:
Note: Only a member of this blog may post a comment.